Ndugu!

YAH: MAONESHO YA JUMUIA ZA KIRAIA BUNGENI DODOMA 2007

1. The Foundation for Civil Society ikishirikiana na ofisi Bunge na AZAKI zinapanga kufanya maonesho ya Jumuia za kiraia Bunge Dodoma kwa mwaka 2007. Maonesho ya Jumuia za Kirai kwa wabunge yameshafanyika mara mbili, 2004 na mwaka 2006. Tunawashukuru wote walioweza kushiriki kwenye maonesho hayo na kuwakilisha maswala mbalimbali yanayohitaji ushawishi wa wabunge ile yafanyiwe kazi na kuleta maendeleo yalio tarajiwa. Kwa ujumla maswala hayo yalikuwa yanahusu uboreshwaji wa sera na sheria mbalimbali.

2. Madhumuni ya maonesho ya mwaka huu wa 2007 yatalenga kuimarisha uhusiano wa bunge na jumuia za kiraia na pia kuzidisha juhudi za wabunge za kujenga hoja kulingana na utashi wa wananchi wanaowawakilisha

3.Fomu za mombi kwa AZAKI zitatolewa hivi karibuni. Kwa mandalizi ya mwaka huu tunapendekeza yafuatayo:
     a.. Jumuia za kiraia zianze kujenga hoja thabiti za ushawishi kwa kupata maoni kwa wananchi wao na walengwa wanaowahudumia,

     b.. Pia Jumuia za kiraia zianze kujenga mahusiano na wabunge wa majimbo yao na pia kujenga mahusiano na kamati za bunge kulingana na hoja wanazotarajia kuziwakilisha na,

     c.. Kupanga mikakata ya ushawishi wakati wa maonesho na pia baada ya maonesho na jinsi ya kupeleka hoja kwenye kamati za bunge na hatimaye bungeni.

4. Mwisho, tunaomba kupata maoni yenu kuhusu mikakati ya kuboresha maonesho ya mwaka huu.

Tunaomba Jumuia za kiraia zilizoshiriki maonesho ya mwaka 2004 na 2006 wawakilishe ripoti fupi kuhusu matokeo ya hoja walizowakilisha na mabadiliko yaliyojitokeza. Pia kutuarifua changamoto walizopata na mipango yao ya baadaye.

Tunategemea ushirikiano wenu.

Deogratius Mlay
The Foundation For Civil Society
Idara ya maendeleo