Sharing With Other People Network
TNC features and provides links and news stories on Tanzania
Search Archive
Keywords:
Search In:
 
News Categories
HOME
BUSINESS & ECONOMY
EDUCATION
E-GOVERNMENT
ENTERTAINMENT
ENVIRONMENT
GOVERNMENT
HEALTH
ICT FOR DEVELOPMENT
RECREATION & SPORTS
SOCIAL SCIENCE
SOCIETY & CULTURE
TOURISM

,Tanzania ,TEKNOHAMA zasaidia wakulima wa Magu kupata masoko bora

TEKNOHAMA zasaidia wakulima wa Magu kupata masoko bora

Na Aloyce Menda

Mengi yamekwisha semwa kuhusu faida za Teknolojia za Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA) katika kuboresha maisha ya binadamu. Pamoja na hayo, Barani Afrika ambako watu wengi wanaishi vijijini, tatizo kubwa linabakia kuwa ni jinsi gani teknolojia hizi za kisasa, kama simu za kiganjani, vitarishi (kompyuta) na tovuti (Internet) zinaweza kutumiwa kuinua maisha ya wakulima wadogo ambao ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi nyingi za Kiafrika.

Tanzania inafanana na nchi nyingine zinazoendelea hususan za Afrika kwa tatizo la umaskini vijijini na sekta za kilimo kushindwa kutoa mafanikio yanayotarajiwa. Ripoti ya mwaka 2001 ya Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP), inasema kwamba teknolojia za kisasa zinaweza kutumiwa vizuri na kuinua haraka uchumi na maisha ya watu wengi maskini.

UNDP inatahadharisha pia kwamba teknolojia za kisasa hususan bioteknolojia katika kilimo zinatakiwa kutumiwa kwa uangalifu kwani zinaweza kuleta madhara makubwa zikitumiwa hovyo.

Waasisi wa mradi wa CROMABU [www.cromabu.com] walikuwa na wazo hilo toka 1999 lakini ripoti ya UNDP ya 2001 iliwaamsha ari zaidi na wakaamua kuanza mradi huo mwishoni mwa 2001. Lengo kuu lilikuwa ni kukusanya na kusambaza taarifa kuhusu bei za mazao katika masoko ya ndani na nje ya nchi kwa manufaa ya wakulima wadogo wadogo wa Magu.

Licha ya kutiwa ari na ripoti ya UNDP 2001, waasisi wa CROMABU walikuwa na lengo la kupata suluhisho la matatizo ya wakulima baada ya Serikali kujitoa katika shughuli zote za biashara na uzalishaji, kuruhusu mfumo wa soko huria. Miaka ya awali ya 1990 ilikuwa na mabadiliko mengi ya kisiasa na kiuchumi duniani na Tanzania ilikumbwa na upepo wa mabadiliko na kuachana na sera nyingi za kijamaa.

Wafadhili wa kimataifa hususan Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), walikuwa wanaweka masharti ya kufanyanyika mabadiliko katika sera mbalimbali za nchi maskini ili ziweze kupata mikopo. Miongoni mwa masharti ilikuwa ni kuwepo kwa masoko huru na mifumo mipya ya usimamizi wa sekta mbalimbali.

Serikali Kuu za zile za mikoa na mitaa zilianza kulegeza udhibiti wa masoko na kuruhusu wafanyabiashara kununua mazao kwa bei ya mapatano na wakulima. Wafanya biashara pia waliruhusiwa kuuza pembejeo kwa bei yoyote wapendayo na hivyo kutumia kila aina ya ujanja na hila kupata faida kubwa. Hali hiyo ilisababisha bei za mazao kushuka sana wakati bei za pembejeo zikipanda mno. Hatimaye wakulima wenye dhamana ndogo walianza kudidimia zaidi katika umaskini, na kusababisha uzalishaji katika kilimo kushuka.

Kilimo ambacho ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania toka miaka ya 1960 kiko katika hali mbaya na mchango wake hivi sasa ni asilimia 50 tu ya pato la taifa ingawa sekta ya kilimo inaajiri asilimia 70 ya nguvukazi yote ya Tanzania. Kwa mujibu wa takwimu za Serikali pato la jumla la kilimo linaongezeka kwa asilimia 3.5 kwa mwaka toka 1981. Mfumo wa sasa wa masoko ya mazao unakatisha tamaa wakulima wadogo ambao ndio wazalishaji wakubwa wa taifa. Hta wakulima wakubwa wachache hawajaridhishwa na sera za kilimo na biashara za hivi sasa.

Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo, sekta ya kilimo inakabiliwa na matatizo mengi, yanayokwamisha maendeleo yake. Tatizo kuu ni wakulima na kilimo kwa ujumla kutothaminiwa na kupewa hadhi yake inayostahili. Maeneo ya mashamba yanayozalisha kwa wingi hayana miundombinu bora, wakulima hawana sehemu za kupata mikopo kwa ajili ya uzalishaji, wanashindwa kupata hati miliki za ardhi na pia hutozwa kodi zinazowaumiza.
Kwa ukubwa wake wa eneo (kilomita za mraba 937,062), Tanzania ina wastani wa hekari 43 milioni zinafaa kwa kilimo, ambazo zinaweza kulisha nusu ya Bara la Afrika zikitumiwa vizuri. Hta hivyo ni wastani wa hekari 6.3 milioni tu zinazolimwa kila mwaka tena na wakulima wadogo wanaotumia zana duni. Mashamba ya wakulima wakubwa sio mengi na yanachukua silimia nne tu ya mashamba yote nchini.

Wakati wadau wa sekta ya kilimo wanadai mabadiliko ya sera kuweka mfumo wa haki wa ushindani katika masoko ya mazao na pembejeo, CROMABU imeanza kuweka sawa masoko kwa kutumia TEKNOHAMA.

Ikiwa na makao makuu wilayani Magu kusini mwa Ziwa Viktoria mkoani Mwanza, CROMABU inafadhiliwa na taasisi ya Kiholanzi ya kuendeleza mawasiliano iitwayo kwa kifupi cha Kiingereza, IICD. CROMABU inaongozwa na meneja mwanamke, Bibi Naomi Massele, chini ya Bodi ya Wakurugenzi inayojumuisha wataalamu wa biashara, kilimo na TEKNOHAMA. Mwaka huu mradi huo unaazimisha mwaka wa nne na umeshapata mafanikio ya kuridhisha.

Kwa mujibu wa Bibi Masele, CROMABU ina sehemu kuu tatu. Sehemu ya kwanza ni Tovuti (Internet) chenye vitarishi (kompyuta) za kutumia kwa kulipia kwa masaa (Internet Cafι). Sehemu ya pili ya kutoa mafunzo kwa jamii ya Magu na sehemu ya tatu ni ya kukusanya na kusambaza taarifa kuhusu hali ya masoko na bei.

Vijana wa Magu, hususan waliomaliza shule za msingi na sekondari wanatumiwa kufanikisha mawasiliano kati ya CROMABU na walengwa wa mradi, ambao ni wakulim wadodo wadogo. Taarifa kuhusu hali ya masoko na bei zinazokusanywa kutoka katika masoko ya Magu na maeneo jirani zinatayarishwa kama ripoti ndogo na kusambazwa. Pia taarifa ya bei za mazao katika masoko ya duni zinazotafutwa kwa kutumia Tovuti zinaandaliwa kama ripoti na kusambazwa. Vijana wanatumia baiskeli za mradi kuwafikia walengwa katika vijiji 16 vinavyopata taarifa moja kwa moja.

Njia nyingine ya mawasiliano ni kwa kupitia sehemu ya mafunzo ya mradi. CROMABU inatoa elimu ya kilimo na biashara kwa vijana wa Magu. Viajana wanaopata mafunzo haya wanatumika pia kusambaza taarifa vijijini wanakotoka.

CROMABU inafikia mwisho wa hatua ya kwanza ya kujisimika ifikapo mwakani 2006 na mradi huo unafahamika kwa wafadhili IICD kama mradi wa mfano utakaoonesha njia kwa wakulima wa maeneo mengine jinsi ya kutumia TEKNOHAMA kujiletea maendeleo.

MWISHO

direct lender payday loans
same day payday loans
quick payday loans with small commissions
easy payday loans and secure !
easy payday loans and secure !
guaranteed payday loans
payday loans lenders online
USER
Welcome back, !
My Profile
Log Out
Main Links
About Us
Submit News
Contact Us
Subscribe
Subscribe to receive news alerts.

Subscribe
Unsubscribe
   
CALENDAR
Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat
31 1 2 3 4 5 6
7 8 9 10 11 12 13
14 15 16 17 18 19 20
21 22 23 24 25 26 27
28 29 30 1 2 3 4
 
2004 - 2006 ©Tanzania Development Gateway, ALL Rights Reserved