Sharing With Other People Network
TNC features and provides links and news stories on Tanzania
Search Archive
Keywords:
Search In:
 
News Categories
HOME
BUSINESS & ECONOMY
EDUCATION
E-GOVERNMENT
ENTERTAINMENT
ENVIRONMENT
GOVERNMENT
HEALTH
ICT FOR DEVELOPMENT
RECREATION & SPORTS
SOCIAL SCIENCE
SOCIETY & CULTURE
TOURISM

,Tanzania ,REPOA YAAZIMISHA MIAKA KUMI YA MAFANIKIO


REPOA YAAZIMISHA MIAKA KUMI YA MAFANIKIO
Mengi ashauri tafiti za utajirisho badala ya kupooza umaskini
* Atoa milioni 100/- kusaidia mabadiliko

Na Aloyce Menda

Matatizo, changamoto na sababu zilizosukuma wasomi kuanzisha chombo cha kutafiti umaskini miaka 10 iliyopita bado yapo. REPOA, ni chombo cha utafiti kilichoundwa mwaka mmoja baada ya warsha iliyofanyika Dar es Salaam, Januari 11, 1994. Ni kifupisho cha maneno ya Kiingereza Research on Poverty Alleviation yakiwa na maana Utafiti juu ya Kupooza Umaskini.

Rais Benjamin Mkapa alikuwa ni waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, wakati alipokaribishwa kama mgeni rasmi katika warsha hiyo iliyobuni REPOA. Katika hotuba yake kwenye warsha, Mkapa alisisitiza umuhimu wa utafiti katika maendeleo na kutaja masuala muhimu kuhusu kiwango cha utafiti hapa Tanzania.

Aliwaambia washiriki wa warsha kwamba ushauri wa kitaalamu wa muda mfupi umekua unachukua nafasi muhimu ya utafiti wa muda mrefu katika kutunga sera mbalimbali hapa nchini. Hapa alikuwa ana maana kwamba washauri wa kitaalamu wanaotoa mawazo tu ambayo pengine hayajafanyiwa utafiti wa kina walikuwa wanatumiwa zaidi na Serikali katika kutengeneza sera mbalimbali badala ya kazi za utafiti na watafiti halisi. Jambo hilo sio zuri na kwa mantiki hiyo alikuwa anatoa changamoto kwa wasomi kuanza kufanyia utafiti masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ili kazi zao ziweze kutumika katika kubuni sera.

Alisema Waafrika tupo nyuma katika maendeleo kwa sababu hatufanyi mambo kisayansi, na pia tunatumia teknolojia duni katika uzalishaji mali. Alionya kwamba bila kuweka kati sayansi na teknolojia muafaka katika shughuli za maendeleo tunazofanya kila siku basi itachukua miongo mingi sana kuondo umaskini mkali unaowakabili watu wengi katika bara hili.

Mwaka mmoja baada ya warsha hiyo, REPOA ilisajiliwa rasmi kama chombo huru cha utafiti, kisicholenga kupata faida wala kufungamana na chama chochote cha siasa, dini, au serikali. Warsha ya kwanza ya utafiti ilifanyika Aprili 1995 na REPOA ikaendeleza ratiba yake kuwa na warsha moja kila mwaka toka wakati huo. Aprili 08 mwaka huu REPOA ilifanya warsha ya 10 ikienda sambamba na maadhimisho ya miaka 10 ya kuundwa kwa chombo hicho.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Kupunguza Umaskini, Mheshimiwa Edgar Maokola-Majogo, alisema katika sherehe za REPOA kutimiza miaka 10 kwamba taasisi hiyo imetoa mchango mkubwa sana katika maendeleo ya taifa hususan katika kupunguza umaskini.

Alisema licha ya tafiti zake kutumiwa kutunga sera mbalimbali na utekelezaji wake, REPOA imeshiriki kikamilifu katika kazi mbalimbali za Serikali kuleta maendeleo na kupunguza umaskini. Alitaja Mpango wa Taifa wa Maendeleo hadi 2025; Mkakati wa Taifa wa Kumaliza Umaskini (NPES); Mkakati wa Ufadhili kwa Tanzania (TAS); Mkakati wa Kupunguza Umaskini (PRSP); na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA) kama baadhi ya kazi nyeti ambazo REPOA ilishiriki kikamilifu.

Pamoja na kauli hizo nzuri, za Waziri Maokola-Majogo, awali Profesa Issa Shivji alisema katika warsha kwamba tatizo la Serikali kutegemea zaidi ushauri wa kitaalamu wa muda mrefu, badala ya tafiti zilizofanywa muda mrefu bado lipo. Profesa Shivji na mkufunzi wa sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na alialikwa katika warsha na sherehe.

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Bwana Reginald Mengi alishauri viongozi wa REPOA kuanza kutafiti jinsi ya kutengeneza utajirisho, baada ya kutimiza miaka 10 ya mafanikio katika kutafiti jinsi ya kupooza umaskini.

Akiongeka kama mgeni mualikwa katika sherehe hizo zilizofanyika hoteli ya Kunduchi mjini Dar es Salaam, Bwana Mengi alisema maneno kupooza umaskini yanasononesha na kukatisha tamaa. Maneno hayo pia hayana msingi wa kisayansi kwani yanaugeuza umaskini kuwa kama kitu cha kudumu kinachohitaji kupoozwa tu kwa muda, alitahadharisha Bwana Mengi na kushangiliwa sana na washiriki wote wa warsha na sherehe.

Akitoa mifano, Bwana Mengi alisema mtu akienda vijijini na kuwaambia watu wa kawaida kwamba amekuja kwao kutafuta njia ya kupunguza umaskini watashindwa kushirikiana naye vyema kwa sababu wataona anawadharau. Lakini mtu huyo huyo akiwaambia watu hao kwamba anataka kushirikiana nao katika kutafuta utajiri, hawatasita kushirikiana naye.

Mengi alisema pia mtu huyo huyo akisafiri hadi Marekani na halafu akakutana na matajiri wa huko na kuwaambia anatafuta ushirikiano wao katika kupunguza umaskini Tanzania, watamkwepa. Lakini akisema anatafuta washirika wa kusaka utajiri, matajiri hao watamsikiliza na kumuunga mkono.

Mengi aliahidi kutoa mchango wa shilingi milioni mia moja kwa REPOA ili ianze kutafiti namna ya kutafuta utajiri. Alishauri pia REPOA ibadilishe jina lake na kuwa Taasisi ya Kutafiti Utajirisho (TAKU).


Alisema jina jipya litawiana na mfumo mpya wa utendaji wenye kulenga katika kutafiti njia za kutengeneza utajiri na litakuwa na mvuto zaidi kwa wadau katika sekta ya binafsi wote wenye kutafuta utajirisho.

Profesa Yodan Kohi, ambaye ni mkurugenzi mkuu wa Komisheni ya Sayansi na Teknolojia aliafiki mawazo ya Mengi ya kubadili jina na REPOA. Alisema anaafiki hivyo wakati akitoa hotuba ya shukrani kwa wageni waalikwa katika sherehe. Profesa Kohi ni mjumbe wa Bodi ya REPOA.

Awali Waziri Maokola-Majogo alisema Bwana Mengi ni profesa wa kutafuta utajirisho na hivyo anastahili shahada ya juu ya heshima kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya REPOA, Profesa Esther Mwaikambo alikataa kusema lolote kuhusu maoni ya Bwana Mengi kutaka REPOA ibadili jina. Lakini Profesa Idris Kikula ambaye ni mjumbe wa Bodi ya REPOA alisema hilo ni jambo lisilowezekana
Katika siku mbili za warsha iliyotangulia sherehe, kazi 34 za utafiti zilijadiliwa na wasomi mbalimbali. Kati hizo kuna ambazo zimekamilika na nyingine ambazo bado utafiti unaendelea.
MWISHO


direct lender payday loans
same day payday loans
quick payday loans with small commissions
easy payday loans and secure !
easy payday loans and secure !
guaranteed payday loans
payday loans lenders online