PROCEDURES
FOR REGISTRATION OF NON GOVERNMENTAL ORGANIZATIONS UNDER THE
NON GOVERNMENTAL ORGANIZATIONS ACT, NO. 24/2002
TARATIBU ZA USAJILI WA NGOs
CHINI YA SHERIA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs) NA.
24 YA MWAKA 2002
Maombi ya usajili wa Mashirika Yasiyo
ya Kiserikali yatakuwa na viambatanisho vifuatavyo kama ilivyopendekezwa
na Sheria hii katika kifungu cha 12(2)
a) Katiba ya Shirika lisilo la Kiserikali
b) Taarifa yenye majina na saini za wanachama waanzilishi
c) Maelezo binafsi ya wanachama na picha
d) Ada ya usajili
e) Anuani na sehemu yalipo makao makuu ya ofisi za Shirika
Lisilo la Kiserikali
f) Maelezo yoyote au taarifa kama itakavyohitajiwa na Msajili
Maombi ya usajili wa Shirika Lisilo la
Kiserikali yatakuwa kwenye fomu maalum NGO A form No. 1
Maombi ya Cheti cha ukubalifu (certificate of Compliance)
yatakuwa na viambatanisho vifuatavyo: -
a) Kivuli halisi cha Katiba ya Shirika
Lisilo la Kiserikali.
b) Cheti cha usajili chini ya Sheria nyingine tofauti na Sheria
ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
c) Taarifa yenye majina na saini za wanachama waanzilishi.
d) Maelezo binafsi ya wanachama na picha
e) Anuani na sehemu yalipo makao makuu ya ofisi za Shirika
Lisilo la Kiserikali.
f) Maelezo yoyote au taarifa kama itakavyohitajiwa na Msajili.
Maombi ya Cheti cha ukubalifu yatakuwa kwenye fomu maalum
NGO A form No, 3.
ADA
Ada ya usajili ngazi ya Wilaya itakuwa ni Shs 41,500/= kama
ifuatavyo:
- Ada ya faili 15,000/ =
- Ada ya usajili 25,000/=
- Stamp duty 1,500/=
Ada ya usajili ngazi ya Mkoa itakuwa ni
Shs 56,500/= kama ifuatavyo:
- Ada ya faili 15,000/=
- Ada ya usajili 40,000/=
- Stamp duty 1,500/=
Ada ya usajili ngazi ya Taifa itakuwa
ni Shs 66,500/= kama ifuatavyo:
- Ada ya faili 15,000/=
- Ada ya usajili 50,000/=
- Stamp duty 1,500/=
Ada ya Mashirika ya Kimataifa itakuwa
ni USD 267 kama ifuatavyo:
- Adayafaili US$ 15
- Ada ya usajili US$ 250
- Stamp duty US$ 2
Kila Shirika lisilo la Kiserikali lililosajiliwa na kupatiwa
cheti cha ukubalifu chini ya Sheria hii, linatakiwa kulipa
ada ya mwaka ya Shs. 50,000/= au US$ 60 kwa Mashirika ya Kimataifa.
Mashirika haya pia yatapaswa kuwasilisha taarifa zake za kazi
za kila mwaka (Annual Report) ambazo zitakuwa kwenye Fomu
maalumu NGO A Form Na. 10 kwa Msajili Mkuu kupitia kwa Wasajili
Wasaidizi.
Mashirika ya Kitaifa na Kimataifa yatasajiliwa moja kwa moja
na Msajili Mkuu. Taratibu zake zitakuwa kama zilivyo taratibu
za usajili katika ngazi nyingine isipokuwa kutakuwa na tofauti
katika ada ya usajili, halikadhalika maombi ya usajili katika
ngazi hizi yatawasilishwa moja kwa moja kwa Msajili Mkuu.
MAMBO MBALIMBALI YA KUZINGATIWA
Utaratibu wa malipo ya ada ya usajili/ mwaka
Malipo ya ada ya usajili wa NGOs na ada za mwaka
yatafanyika kama ifuatavyo:
(i) NGOs zote zitakazosajili katika ngazi ya Mikoa na Wilaya
watalipa fedha katika Akaunti Nambari 16:29 Miscellaneous
Deposit (Akaunti hii ni ya Hazina iliyoko kila mkoa) kwenye
matawi ya Benki ya NMB katika maeneo yao.
(ii) NGOs zitakazosajili ngazi ya
Kitaifa na Kimataifa watalipa fedha zao katika Akaunti Nambari
16:140 Miscellaneous Deposit (Hazina Ndogo mkoa wa Dar es
Salaam). Kiutendaji Idara ya Uhasibu, Ofisi ya Makamu wa Rais
itapokea fedha hizo na kutoa stakabadhi halali ya malipo hayo.
|